Kamwelwe ameyasema hayo leo Jumamosi Juni 29,2019 jijini Dar es Salaam wakati akifanya ziara bandarini kutembelea mizani ya Shimo la Udongo inayodaiwa kuchelewesha malori yanayokwenda kupakia au kupakua mzigo bandarini.
"Tumefanya utafiti wa siku tatu na kubaini kwamba kuna wamiliki watatu wa ICD wanafanya hujuma kwa kuwaagiza madereva wao wapaki malori kufunga barabara ili magari yasiingie bandarini, hiyo ni hujuma, hatuwezi kuwaacha. Lazima nichukue hatua."
"Labda niwaambie tu kwamba hizi mizani haziondolewi hapa, zimewekwa ili kudhibiti kiwango cha mzigo kinachopita kwenye barabara zetu. Tutakachofanya ni kuboresha mazingira ili magari yatoke kwa haraka zaidi," amesema waziri huyo.
Amesema yoyote atakayezuia magari kuingia kwenye mizani kwa madai kwamba mizani ni mbovu, watachukuliwa hatua kali. Amesisitiza kwamba mizani zote mbili ni nzima na zinafanya kazi kama kawaida.
Amesema kitendo kilichofanyika jana usiku cha madereva kuzuia malori kuingia kwenye mizani ni hujuma kwa Taifa kwa sababu bandari ni mpaka kama mipaka mingine na inadhibitiwa na serikali, siyo mtu mwingine.
Hali ya usafiri bandarini hapo inaendelea kama kawaida licha ya kwamba bado kuna msongamano mkubwa wa malori yanayoingia kwenye mizani kupima uzito wa mzigo.
No comments:
Post a Comment