Leo June 29, 2019 Waziri wa Madini Dotto Biteko, amewataka wachimbaji madini wasiokuwa waaminifu waachane na kazi ya uchimbaji wa madini na badala yake, waendelee na kazi zingine kwani wizi wa madini sasa ni zilipendwa.
‘‘Niwaombe wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini na wenye roho za wizi, wizi wa madini sasa ni zilipendwa utakuwa unatafuta vitu viwili tu Jela au umasikini, sisi tusingependa kuona Mtanzania anafilisika sababu ya hili jambo, kodi unayolipa ni asilimia 7 pekee” Waziri Biteko
“Watanzania tubadilike tuwe Taifa la watu waaminifu, lipo kundi linatapeli watu huko nje ya nchi sasa ninawaambia siku zenu zinahesabika watu wanakuja kulalamika wanatapeliwa na Watanzania mnatuharibia jina” Waziri wa Madini
“Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kusimamia madini kwa miaka mingi waliokuwa wanachimba ni wageni hivyo Rais ameona uchungu huo na sasa wamepewa Watanzania sasa inashangaza unaona eti bado kuna wanaotaka kuiba” Waziri wa Madini
“Kumekuwa na utoroshwaji wa madini ya Tanzanite kwenda nchi jirani halafu wanasema na wao wanayo madini hayo wakati Tanzanite inapatikana Tanzania tu hivyo hatuwezi kuendelea kulifumbia mbacho suala hili”Katibu Mkuu Hazina
“MUNGU alitupa madini mbalimbali tofauti na nchi nyingine miaka ya nyuma hata Mwalimu Nyerere alikua anasema pale Mwadui tumebaki na madini ya miaka saba tu lakini sayansi inasema tuna madini ya zaidi ya miaka 100″ Waziri Mahiga
“Haiwezekani watu wanapora mali zote hizi, sijui tungejenga Zahanati ngapi kupitia fedha hizi, kuna watu wanalalamika hakuna maji lakini wengine wanapora huu utajiri wetu, sisi sio masikini” Waziri wa Fedha
“Tukio hili la leo limenifurahisha sana kwani tuna mahitaji mengi sana Watanzania hivyo fedha hizi tutazitumia katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo kama vile ujenzi wa barabara, shule, zahanati” Waziri wa Fedha
“Wanaotuhujumu sasa basi hakuna nafasi tena na niwaombe Mahakama na Vyombo vya Dola msiwe na huruma na hawa watu washughulikiwe kikamilifu kwani hawa ndio wanaorudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu”Waziri wa Fedha
“Watanzania wenzangu tusaidie vyombo vyetu vya usalama maana hizi ni mali zetu wote hivyo tuwe macho kuhakikisha tunawaumbua hawa watu wenye nia ovu” Waziri wa Fedha
“Mali hii iko salama na sisi tunawahakikishia kwamba Serikali ikishafanya uamuzi tutatumia mali hii katika kusaidia Watanzania, hivyo niwaombe tusaidiane kuhakikisha nchi yetu inakwenda mbele,” Waziri wa Fedha
No comments:
Post a Comment