We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, June 29, 2019

Mama na mwanaye wanyolewa kipara baada ya kukataa kubakwa


Jeshi la Polisi nchini India linawashikilia watu wawili katika jimbo la Bihar kwa tuhuma za kuwanyoa kipara wanawake wawili baada ya kugoma kubakwa.
Watuhumiwa hao na wengine ambao walikimbia wanadaiwa kuvamia nyumba ya mwanamke huyo (jina limehifadhiwa) aliyekuwa amelala na mwanaye kwa nia ya kuwabaka lakini walishindwa na kuamua kuwapa adhabu ya kuwanyoa vipara.
"Wanaume hao waliingia kwenye nyumba ya mwanamke huyo na kujaribu kuwanajisi lakini mama alipamba na wabakaji hao,” ilisema taarifa ya polisi.
Kwa mujibu wa Shirika la habari la Ani, wabakaji hao waliwashambulia kisha kuwatoa nje kwa kuwatembeza mtaani kabla ya kuwanyoa nywele zote mbele ya wanakijiji
"Walituchapa hovyo na fimbo, nina majeraha mwili mzima. Binti yangu pia ana majeraha,” alieleza mama huyo.
Hata hivyo, polisi nchini humo imesema kuwa bado inawasaka  wanaume wengine watano waliohusika kwenye tukio hilo.
Kujaribu kubaka ni kosa la kijinsia nchini India lakini matukio ya ubakaji yanazidi kuongezeka.
Hii si mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea kwenye Jimbo la Bihar, Aprili, mwaka huu msichana mmoja alishambuliwa kwa tindikali baada ya kugoma kubakwa na kundi la wanaume.
Miezi michache kabla ya tukio hilo, mwanamke mwingine alishambuliwa kisha kuvuliwa nguo zote na kutembezwa akiwa uchi katikati ya soko la kijiji.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list