Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema anatarajia Bunge au Serikali kuchukua hatua kwa kauli aliyoitoa Mbunge Lusinde juu ya Wakenya kupigwa kama kujibu mapigo ya kauli la Jaguar.
Lema amesema yeye amefukuzwa Bungeni kwa vikao vyote mpaka 2020 kwa kuunga mkono kauli ya CAG na Halima Mdee juu ya udhaifu wa Bunge.
"Nimefukuzwa Bungeni kwa vikao vyote mpaka mwaka 2020,kwa kuunga mkono kauli ya CAG/Mh Mdee juu ya udhaifu wa Bunge, natarajia Bunge/Serikali kuchukua hatua kwa kauli aliyoitoa Mb L.Lusinde, juu ya Wakenya kupigwa kama kujibu mapigo kauli ya Mb Jaguar.Hili ni jaribu baya kwa EAC," ameandika Lema kwenye mitandao yake ya Kijamii.
Lema na Halima Mdee walisimamishwa kutohudhuria vikao vya Bunge kwa kuunga mkono kauli ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.

No comments:
Post a Comment