Aliyekuwa kocha wa AS Kigali Masudi Djuma amesema Yanga imepata mchezaji hasa baada ya kumsajili kiungo mshambuliaji Issa Bigirimana kutoka APR ya Rwanda
Djuma aliyewahi kufanya kazi Tanzania na klabu ya Simba, amesema anamfahamu Bigirimana vizuri na anaamini atapata mafanikio makubwa katika klabu ya Yanga
Djuma amesema kuwa anatambua uwezo wa mchezaji huyo, akiwa ameibuka mfungaji bora zaidi ya mara nne timu ya APR, hivyo anaamini atafanya mambo mazuri pia kwa Wanajangwani hao.
"Nimekuwa na Bigirimana katika timu zaidi ya tatu na nimekutana naye tena hapa APR, Rwanda, natambua uwezo wake ni mzuri, pia ni mchezaji ambaye anajiamini sana anapokuwa uwanjani," Djuma amenukuliwa na gazeti la Bingwa
"Hata hivyo, niliposikia anakuja Tanzania kujiunga na klabu ya Yanga, niliona wamepata kiungo mzuri ambaye atawasaidia kwenye plani zao"
"Bigirimana ni kama mdogo wangu, baada ya kufahamu anakuja Tanzania nimezungumza naye mambo mengi, lakini nimemsisitiza zaidi kufanya kazi nzuri ili azidi kijitengenezea njia ya kufika mbali"
Katika klabu ya Yanga, Bigirimana atakuwa na kiungo mwingine mshambuliaji Patrick Sibomana wakiwa wote wametokea Rwanda

No comments:
Post a Comment