We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, June 28, 2019

Dodoma yakaribisha wawekezaji


Mkoa wa Dodoma umealika wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kutumia uwepo wa fursa lukuki za uwekezaji kuwekeza katika sekta za ujenzi wa viwanda, miundombinu, masoko, kuchakata na kuongeza thamani mazao.

Akitangaza fursa hizo kwenye kongamano la siku mbili la uwekezaji mkoani humo, Katibu Tawala wa Mkoa, Maduka Kessy amesema mkoa umefungua milango kwa wawekezaji wa ndani na nje kuchangamkia fursa nyingi zilizomo katika mkoani huo.

Kessy amezitaja fursa hizo kuwa ni za kilimo cha maembe, alizeti na mazao ya misitu, ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji, mizinga nyuki ya kisasa na ufugaji na uvuvi.

Pia ujenzi wa viwanda mbalimbali hasa vya vifungashio, vya maziwa, ngozi na vyakula vya mifugo.

"Vile vile, vya kuchakata na kuongeza thamani zabibu, alizeti, maembe, taka ngumu, karanga, nafaka, na mpunga. Katika sekta ya elimu wanaweza kuwekeza katika kufungua chuo maalumu cha ujuzi, uwekezaji katika hoteli,"amesema.

Alitaja fursa nyingine kuwa ni ujenzi wa miundombinu ya masoko, uwekezaji katika ujenzi wa maghala, vituo vya mabasi, mji wa kibiashara na maegesho ya magari ya mizigo.

Akizungumza, Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), John Mnali amesema Tanzania ipo kwenye fursa nzuri ya uwekezaji kutokana na mambo mengi yakiwemo ya kijiografia. 

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list