Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alionekana akitetemeka kwa mara nyingine tena mjini Berlin Alhamisi wakati wa hafla mjini Berlin , siku nane baada ya kufanya hivyo.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel aonekana akitetemeka mikono na miguu mbele ya hadhara, ashindwa kunywa maji aliyopewa (+video)
Video inayoonyesha Bi Merkel, 64, akijikunyata kwa mikono yake huku mwili wake ukitetemeka badaa ya dakika kama mbili alionekana kurejea katika hali ya kawaida na akasalimiana kwa mikono na waziri mpya wa sheria wa Ujerumani.
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Alipewa glasi ya maiji ya kunywa, lakini hakuyanywa.
Katika tukio la awali Bi Merkel alisema kutetemeka kwa mwili kulitokana na upungufu wa maji mwilini.
Baadae aliondoka kuelekea katika mkutano wa G20 mjini Japan mchana kama ilivyokuwa imepangwa.
” Mambo yote yanaendelea kama ilivyopangwa. Kansela wa shirikisho yuko salama,” alisema msemaji wake Steffen Seibert.
Shirika la habari la Ujerumani DPA lilisema kuwa licha ya kipindi cha joto nchini humo , joto lilikuwa limepunguwa wakati wa hafla iliyofanyika katika kasri la Bellevue , ambako rais Frank-Walter Steinmeier alikuwa akimtangaza waziri mpya wa sheria Christine Lambrecht.
Mara ya mwisho , Bi Merkel alitetemeka alipokuwa amesima kando ya rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky chini ya jua . Alisema alijihisi vizuri baada ya kunywa maji.
Siku ya Alhamis alihudhuria kuapishwa kwa Bi Lambrecht bungeni (Bundestag) kwa muda mfupi -na baadae akaondoka.
Atakaporejea kutoka Japan, Bi Merkel atakabiliwa na mazungumzo magumu mjini Brussels wakati ambapo yeye na viongozi wengine wa Muungano wa Ulaya kumtafuta mgombea wa urais wa tume ya Muungano wa Ulaya atakayechukua nafasi ya Jean-Claude Juncker.
Anaweza kuwa na tatizo gani?
Duru za serikali zimeviambia vyombo vya habari vya Ujerumani kuwa hakukuwa na cha kuhofia na alipokuwa anaondoka kuelekea Osaka, msemaji wake alituma ujumbe wa tweeter kwamba” mazungumzo ya ushirikiano yamepangwa na wakuu wengine wa serikali na nchi”.
Hata hivyo, Bi Merkel alikuwa na tatizo la kutetemeka wakati wa hali ya hewa ya joto alipokuwa katika zira nchini Mexico mwaka 2017, alipokuwa akihudhuria sherehe za kijeshi.
Alifanyiwa uchunguzi mwingi wa kimatibabu na hakuna tatizo lililopatikana, kulingana na taarifa.
Hakuna ushahidi , kwa mfano wa ugonjwa wa mishipa wa Parkinson ,ambao humfanya mtu kuwa na dalili za kutetemeka kwa mwili.Mikono ya Merkel na miguu ilionekana ikitetemeka
Akihojiwa na mtandao wa Focus juu ya tatizo ambalo linaweza kuwa lilisababisha kutetemeka kwa Bi Merkel Alhamis , Daktari maarufu wa Bavaria Jakob Berger alisema kuwa atahitaji kuchunguzwa haraka iwezekanavyo hata hivyo alisema kuwa hawezi kuwa na maradhi ya Parkinson kwasababu mtetemeko wa mwili wake ulikuwa mkubwa.
Lakini akasema “angekuwa ni mgonjwa wangu ningetambua dalili kabla ya safari yake ya kwenda Japan)”.
Mtaalamu mwingine wa afya Dkt Christoph Specht, ameviambia vyombo vya habari vya Ujerumani kuwa huenda Bi Merkel amepata maambukizi, kwani kutetemeka ni dalili ya maambukizi ambayo yamejitokeza tena. Maambukizi hayo huenda yamesababishwa na kitu kingine, alisema, na Merkel atahitaji kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Merkel anapata huduma gani za matibabu?
Kansela hana daktari wake binafsi lakini anauwezo wa kupata huduma ya tiba ya hali ya juu. Ofisi yake ipo karibu na hospitari ya kijeshi ya Charité hospital and the military hospital mjini Berlin, na Kansela na uwezo wa kupata matibabu kutoka kwa madaktari wa ngazi ya juu.
Msemaji wa serikali alikataa kuzungumzia huduma yoyte ya matibabu aliyopatiw, lakini huenda alipata huduma ya matibabu alipokuwa katika safari yake ya Japan kwani madaktari wa Wizara ya mashauri ya kigeni huambatana wakati wote na ujumbe unapokwenda katika ziara kubwa za mataifa ya kigeni.Bi Merkel , katikati, akionekana katika hali nzuri muda mfupibaadae
Kwa sasa Bi Merkel anahudumu kwa muhula wa nne wa Ukansela, kazi aliyoianza Novemba 2005. Amesema kuwa ataacha siasa muhula wake utakapomaliza muhula wake wa sasa mwaka 2021.
Amekuwa na afya nzuri katika kipind chote alichokuwa mamlakani, na hata amekuwa kifanyia kazi nyumbani baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti mwaka 2011; alianguka alipokuwa akicheza mchezo wa kuteleza kwenye barafu mnamo mwaka 2014. mama yake alifariki mapema mwaka huu.
Angebainika kutokuwa na uwezo wa kutkeleza majukumu, Naibu Kansela Olaf Scholz angeingilia kati. Kwa sasa ni waziri wa fedha , na yuko katika chama cha mreko wa kati-kushoto cha and is in the centre-left Social Democratic (SPD), am,bacho ni chama chenye shirika katika muungano wa CDU.
Ni Kansela aliyehudumu kwa muda mrefu nchini Ujerumanibaada ya vita . Rekodi iliwekwa na mtangulizi wake kutoka chama cha mrengo wa kati- kulia cha Christian Democrat , Helmut Kohl ambaye alihudumu kwa zaid ya miaka 16 akiwa ni wa pili kwa Konrad Adenauer (zaidi ya miaka 14 ).
No comments:
Post a Comment