Beki kisiki wa Simba Paschal Serge Wawa ameanza mazoezi mepesi tayari kurejea dimbani baada ya kuwa nje kwa zaidi ya wiki tatu
Wawa aliumia kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kati ya Simba dhidi ya TP Mazembe uliopigwa uwanja wa Taifa
Wawa ameanza mazoezi binafsi na huenda akajumuishwa kwenye kikosi cha Simba kitakaporudi kutoka mkoani Mbeya
Mwenyewe amethibitisha kuwa hali yake inaendelea vizuri na tayari ameshaanza mazoezi binafsi
"Ninaendelea vizuri kwa sasa tofauti na awali na nimeanza mazoezi binafsi na sasa hivi ninafanya mazoezi ya Gmy," amesema
Simba imecheza michezo sita ya ligi bila ya Wawa na imefanikiwa kushinda michezo mitano
Walinzi Juuko Murshidi, Paul Bukaba na Yusufu Mlipili wameweza kutimiza ipasavyo majukumu ya ulinzi wa kati wakishirikiana na mkongwe kiraka Erasto Nyoni
No comments:
Post a Comment