Na Amiri kilagalila –Njombe
Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA mkoani Njombe limekemea baadhi ya wanasiasa kutumia majukwaa ya kisiasa kuingilia matatizo ya kiutumishi.
Hayo yametolewa na mratibu wa TUCTA mkoa wa Njombe Fraten kwaison wakati akisoma taarifa ya shirikisho mbele ya mamia ya watumishi wa sekta binafsi na sekta za umma katika viwanja vya CCM vilivyopo kata ya Ilembula wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kimkoa yaliyofanyika wilayani hapo.
“Kuna baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitumia vibaya majukwaa ya wanasiasa kuwadhalilisha watumishi wa uma kwa kuegemea maelezo ya upande mmoja bila kupata maelezo ya upande wa pili,kitendo hiki kimekuwa kikishusha molali ya kazi kwa baadhi ya watumishi,vyama vya wafanyakazi vinakemea vitendo hivi vya udhalilishaji”alisema mratibu wa Tucta mkoa wa Njombe
Aidha mratibu amesema watumishi wanaongozwa na sheria,kanuni na taratibu hivyo pindi yanapotokea matatizo ya kiutumishi ni vema kutatuliwa na waajili wao na sio wanasiasa.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Ally Kasinge kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Olesendeka,amepiga marufuka wanasiasa na viongozi wa kisiasa kwa nafasi zao mkoani humo kuingilia majukumu ya kiutumishi kwa kuwa utumishi wa umma unaongozwa kwa mujibu sheria kanuni na taratibu kupitia mamlaka zao.

No comments:
Post a Comment