Na Timothy Itembe - Mara
Mkuu wa mkoa Mara, Adamu Kigoma Malima ameonyesha kusikitishwa na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto vya Ubakaji, huku wengine wakilawitiwa hali ambayo inasababisha kuwaathiri kijamii.
Alisema kuwa ofisini kwake kesi zaidi ya 12 zimeripotiwa za kubakwa watoto huku baadhi ya kesi hizo zikiripotiwa kuwa zimetendwa na baadhi ya watu wenye utovu wa nidhamu ndani ya Taifa letu wengine wanaotajwa ni waalimu wa shule za misngi na sekondari.
RC Malima alisema hayo jana katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani ambayo kwa mkoa Mara yalifanyikia ndani ya viwanja vya Chuo Cha uwalimu TTC mjini Bunda.
“Ofisini kwangu kumeripotiwa kesi za ubakaji zaidi ya 12 baadhi zikiwa zinahusisha walimu wa shule za misngi na sekondari niwaombe ndugu zangu haki ya kufanya kazi bila kubugudhiwa ni ya msingi lakini niwatake kuacha vitendo vya Rushwa ya Ngono kazini pamoja na vitendo vya ubakaji watoto wa shule”alisema RC Malima.
Kwa upande wake mwenyekiti wa TALWGU mkoani Mara, Kalebu Kihongo alisema kuwa wafanyakazi wanachangamoto nyingi ikiwemo ya watumishi kutolipwa fedha za mafao yao kwa wakati pindi wanapostaafu hali ambayo inasababisha waishi katika mazingira magumu.
Naye mwenyekiti wa Chama cha walimu mkoa Mara, Mwalimu Livingstoni Gamba aliwataka walimu pamoja na wafanyakazi kwa ujumla kuchukua wajibu wa kufanyakazi kama sheria inavyowataka.

No comments:
Post a Comment