Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt Reginald Abraham Mengi (75) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa jijini Dubai, katika Falme za Kiarabu (UAE).
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dk Mengi aliandika Aprili 10 kuwa yupo nchini India kwa ajili ya kupandikiza vinasaba (stem cell and genetic engineering), huku akiomba watu kumuombea ili kuweza kufanikisha matibabu hayo.
Alizaliwa mwaka 1944 mkoani Kilimanjaro, na ana watoto watano ambao ni Regina, Rodnay, Abdiel, Jayde na Ryan. Watoto hao amezaa na Mercy Mengi pamoja Jackline Mengi.
Dk Mengi alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa barani Afrika, ambapo sehemu ya utajiri wake aliuelekeza kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes mwaka 2014, utajiri wa bilionea huyo ulitajwa kuwa ni TZS trilioni 1.3 ($560 milioni).
Enzi za uwahi wake na katika shughuli zake aliweza kushinda tuzo mbalimbali za kitaifa na kimataifa, pamoa na kuandika kitabu chake cha I Can, I Must, I will.
Kifo cha Dk Mengi kimetokea ikiwa ni miezi 6 tangu mke wake wa kwanza, Mercy Mengi alipofariki. Mercy Mengi alifariki dunia usiku wa Novemba 1,2018 katika Hospitali ya Mediclinic Morningside Afrika Kusini akipatiwa matibabu.

No comments:
Post a Comment