Kamisheni ya Mawasiliano nchini Uganda UCC imetoa agizo la kusimamishwa kazi mara moja kwa waandishi na watayarishaji 39 wa vipindi vya televisheni, wakuu wa vipindi pamoja na wakuu wa vitengo vya habari chini humo wanofanya kazi kwenye vituo sita binafsi vya televisheni.
Sambamba na hilo vituo saba vya redio vimechukuliwa hatua dhidi ya urushaji wa maudhui ya kichochezi.
Japokuwa kamisheni hiyo haikuweka wazi sababu za kutaka hatua hizo zichukuliwe, Imebainika kwamba sababu kuu ni urushaji wa matangazo ya kuzuiwa na kukamatwa kwa wafuasi wa upinzani akiwamo Mbunge Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine.

No comments:
Post a Comment