Wakati wa michuano ya SportPesa Super Cup, beki Lamine Moro raia wa Ghana aliitumikia Simba, akicheza mechi zote za timu hiyo
Katika michuano hiyo, klabu ya AFC Leopards ilimuwekea pingamizi beki huyo kutokana na leseni yake kuonekana ni mchezaji halali ya wa Buildcon FC ya Zambia
Hata hivyo pingamizi hilo lilitupiliwa mbali
Juzi Lamine nae alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga
Ujio wa Lamine umefanikishwa na kocha Mwinyi Zahera ambaye kabla ya kutua Yanga aliinoa kwa kipindi kifupi klabu ya Buildcon na kuvutiwa na uwezo wa mlinzi huyo wa kati
Wakati huu Yanga inaendelea na mazungumzo na mshambuliaji Mzambia Kalengo Maybin aliyetokea klabu ya ZESCO United
Mzambia huyo tayari yuko nchini akitarajiwa 'kusinya' mkataba wa miaka miwili kuchukua nafasi ya Heritier Makambo aliyetimkia Horoya AC

No comments:
Post a Comment