Baada ya kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la FA (ASFC) kikosi cha Yanga kinaondoka jijini Mwanza asubuhi ya leo Jumapili kurejea jijini Dar es salaam tayari kwa safari ya Mtwara
Yanga inakabiliwa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Ndanda Fc utakaopigwa Jumatano, April 03 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara
Kikosi cha kocha Mwinyi Zahera kimepania kushinda mchezo huo ili kuendea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi
Yanga inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama 67, ikifuatiwa na Azam Fc yenye alama 59
Simba inayoshuka dimbani mkoani Morogoro leo kuchuana na Mbao Fc, inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 54

No comments:
Post a Comment