We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, March 31, 2019

Serikali yasisitiza, uchaguzi Yanga ndani ya siku 30, yawaonya wanaoanzisha migogoro


Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini Yusuph Singo ameliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhakikisha uchaguzi wa Yanga unafanyika ndani ya siku 30
Singo amesema anafahamu migogoro iliyokuwepo huko nyuma katika klabu ya Yanga imeshafika tamati hivyo hakuna sababu ya uchaguzi huo kutofanyika katika muda uliopangwa

Amewatahadharisha viongozi, wapenzi na wanachama wa Yanga kutoanzisha migogoro na vikwazo zaidi ili uchaguzi huo uweze kufanyika
Tamko hilo la Serikali limekuja siku moja baada ya Mwanachama maarufu wa Yanga Mzee Ibrahim Akilimali kuibuka na kupinga tarahe ya uchaguzi iliyotangazwa na Bodi ya Wadhamini ya Yanga, pia akipinga Kamati iliyoundwa kuisimamia timu kuelekea uchaguzi

Yanga imetangaza kufanya uchaguzi April 28 2019 baada ya viongozi wake wote kujiuzulu.
Kwa sasa timu inasimamiwa na Kamati Maalum iliyoundwa

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list