Baada ya kupenya hatua ya nusu fainali michuano ya kombe la FA (ASFC), kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema mchezo wa nusu fainali dhidi ya Lipuli Fc utakuwa mwepesi, ana matumaini makubwa kuwa kikosi chake kitatinga fainali
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo jana, Zahera amesema mchezo dhidi ya Alliance ulikuwa mgumu sana na walihitaji bahati kuweza kusonga mbele
"Leo (jana) tumeteseka sana, michezo miwili tuliyocheza na Alliance hapa Mwanza tumeteseka sana lakini mchezo ujao dhidi ya Lipuli utakuwa rahisi kwetu," alisema Zahera
"Nimewaangalia Lipuli Fc, mchezo waliotufunga tuliwazidi kila kitu lakini tulikosa bahati tu"
"Ukiacha mpira wa adhabu waliyofunga na kona moja aliyodaka Kindoki, hawakutengeneza nafasi zaidi yetu"
"Sisi tulitengeneza nafasi sita lakini hatukuzitumia. Hivyo Lipuli Fc hawatutishi, tutarejea Iringa kucheza nao "
Yanga inatarajiwa kucheza na Lipuli Fc mwishoni mwa mwezi wa nne katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa uwanja wa Samora, Azam Fc itacheza na KMC katika mchezo mwingine wa nusu fainali utakaopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi
No comments:
Post a Comment