Nahodha wa kikosi cha Simba John Bocco 'Adebayor' yuko kwenye kiwango bora sana, leo anatarajiwa kuwaongoza mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara kuikabili Mbao Fc mkoani Morogoro
Baada ya kufanya kazi kubwa ya kuivusha Simba hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vita, kisha akaivusha Stars fainali za AFCON 2019 katika mchezo dhidi ya Uganda kwa kutengeneza mabao mawili kati ya matatu yaliyofungwa na Stars, Bocco leo atakuwa dimbani kufanya kazi maalum ya kuitafutia Simba alama tatu muhimu
Aidha kinara wa upachikaji mabao katika kikosi cha Simba, Meddie Kagere naye atakuwa na nafasi ya kuongeza mabao yake na kumkaribia Salum Aiyee wa Mwadui Fc mwenye mabao 16
Kagere yuko nafasi ya pili kwenye orodha ya vinara wa upachikaji mabao akiwa na mabao 13
Bocco na Kagere wamerejea kikosini baada ya kutumikia timu zao za Taifa wakiwa 'fit' na hakuna shaka Aussems anazihitaji silaha hizi kuweza kuimaliza Mbao Fc baadae leo

No comments:
Post a Comment