We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, March 2, 2019

Waziri Ndalichako atoa neno kwa Wanawake wa Tanzania


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ametoa wito kwa wazazi hususani wanawake kuwa mstari wa mbele kuyasaidia makundi ya watu wasiojiweza na hasa watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili wapate haki zao za msingi hususan elimu.

Prof. Ndalichako ametoa wito huo mkoani Kigoma wakati akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya maombi ya dunia kwa wanawake wa umoja wa wamama wa kikristo Tanzania CCT na kusema kuwa wanawake wakiamua wana uwezo wa kubadili maisha katika jamii.

Amesema wanawake ndio walezi wa watoto kuanzia ngazi za familia akiwafananisha na walimu kwani wao wana jukumu la kulea na kufundisha watoto wote bila kujali ni wa kwake.

"Mama Salma Kikwete ambae ni mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kiwete amewahi kusema kuwa mtoto wa mwenzio ni wa kwako hivyo tuwasaidie watoto yatima, wa mitaani na wale wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kutimiza ndoto zao na hasa kupata elimu," aliongeza Waziri Ndalichako.

Aidha Profesa Ndalichako mewataka kinamama kote nchini kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa vitendo kwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali.

Profesa Ndalichako ametoa wito kwa Watanzania wote hususani wanawake kudumisha mshikamano uliopo Tanzanania kwa kuendelea kufanya maombi na ibada ya kuiombea nchi ya Tanzania na pamoja na viongozi wake.

Profesa Ndalichako pia amefanya ziara fupi ya kutembelea wagonjwa ambao wamelazwa katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Kigoma Maweni na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa hao.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list