We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, March 2, 2019

Serikali yahimiza jamii kupima maambukizi ya VVU


Jamii imeshauriwa kupima afya zao mara kwa mara ili kubaini kama wana maambukizi ya VVU ili kupata huduma mapema na kuchukua hatua muhimu ya kunendelea kulinda afya za wasio na maambukizi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alipokuwa akizindua kituo cha kutolea huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika Mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara Machi1, 2019.

Waziri Mhagama aliwahimiza wananchi kupima VVU  ili kufanikisha mpango wa 90 tatu na kutoa hamasa kubwa kwa wanaume kuwa mstari wa mbele katika kupima afya zao,na wakina mama kisiwe kipimo chao.

“Ili kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi nchini, asilimia 95 ya watanzania ambao hawana maambukizi ya Virusi vya UKIMWI inapaswa walindwe ili wasiambukizwe na kundi la wanaume wawe mstari wa mbele kujitokeza kupima afya zao,”alisema Mhagama.

Waziri aliongezea kuwa ni vyema jamii kuendelea kujilinda ili kuepuka maambukizi mapya yanayosababisha takwimu za maambukizi nchini kuongezeka badala ya kupungua.

“Pia asilimia tano ya watanzania ambao wana maambukizi ya virusi vya UKIMWI inapaswa walindwe ili asilimia hizo zisiongezeke kutokana na mpango wa 90 tatu”, alisisitiza Mhagama.

Alisema pia kwenye asilimia hiyo 90 watakaopima na kukuta wamepata maambukizi wanapaswa kutumia dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ili kuhakikisha maambukizi mapya yanatokomezwa kabisa hapa nchini.

Aliwataka wananchi wa eneo hilo kutumia kituo hicho kwa kutunza afya zao na kuishi kwa furaha kwani kinawahusu wenye maambukizi na wale wanaohitaji kujua afya zao.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti alisema Mirerani ndiyo sehemu inayoongoza kwenye mkoa huo kwa kuwa na watu wengi wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kulinganisha maeneo mengine katika mkoa huo. 

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list