Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Riginald Mengi amesema kuwa Ruge hajafa kwasababu roho haifi kilichokufa ni kasha la mwili wake.
Mengi amesema kuwa Ruge anaishi sehemu mbili kwa Mungu na kwenye roho zetu kwasababu aligusa maisha ya Watanzania wengi.
“Nina habari njema kwenu Ruge hajafa, kwasababu roho haifi kilichokufa ni kasha la mwili wa Ruge na sio roho yake, tunazika mwili wake hatuziki roho yake na kuna siku mtajua kuwa Ruge anaishi na ataendelea kuishi katika roho zetu na kwa baba Mungu,” amesema Mzee Mengi.
Ruge Mutahaba amefariki siku ya February 26 mwaka huu nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment