"Waziri Mpina utakuwaje Waziri wa Mifugo katika nchi ambayo mifugo yake inatangatanga kutafuta soko la nje bora ufukuzwe."
Akizungumza mara kwenye hafla hiyo ya uwekaji jiwe la msingi, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina alisema Serikali haitaogopa lawama katika kulinda rasilimali za nchi, wawekezaji wa ndani, ajira na mapato ya Serikali.
Hivyo aliwahakikishia TANCHOICE na wawekezaji wengine wa mazao ya mifugo kutembea kifua mbele kwani hakuna mtu yoyote atakayechezea soko letu huku akisisitiza kuwa rasilimali za mifugo zitapatikana za kutosheleza mahitaji ya viwanda nchini.
“Utakuwaje Waziri wa Mifugo katika nchi ambayo wananchi wake hawali mifugo yao, utakuwaje Waziri wa Mifugo katika nchi ambayo mifugo yake inatangatanga kutafuta soko la nje huku soko la ndani likiwa limetekwa na bidhaa za mifugo ambazo hata ubora wake haiujathibitishwa ni bora ufukuzwe tu” alisema Waziri Mpina akiwa Kibaha.


No comments:
Post a Comment