Na Enock Magali, Dodoma
Waziri wa Madini Mh.Dotto Biteko amezindua Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) huku akiitaka Bodi hiyo kutoa taarifa sahihi juu ya wachimbaji wadogo,wakati na wakubwa kwa Serikali.
Mh.Biteko amesema kuwa Serikali ilifanya marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2010 kwa lengo la kuhimarisha usimamizi wa Seriakali katika sekta ya madini ambapo katika marekebisho hayo sambamba na kanuni zake za mwaka 2018 Bodi ya GST iliundwa.
Waziri Biteko amefanya uzinduzi huo March 27 mwaka huu Ofisini kwake Jijini Dodoma ambapo pamoja na maelekezo mengine pia amewataka GST kutunza siri za watafiti pindi zinapowasilishwa kwao.
“Lakini pia msisahau watafiti nao lazima wafurahie usiri wa taarifa zinazoletwa kwenu,asitokee mtu GST baada ya kupata taarifa za mteja kwa sababu ametumia fedha nyingi zile data ni mali yake,ameleta Serikalini alafu akatokea mtu ambaye sio mwaminifu akachukua hizo ripoti akaenda kuzitoa nje kwa lengo la kujipatia fedha itakuwa ni bahati mbaya sana”Alisema.
Aidha pia ameongeza kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha inawahamisha wachimbaji katika mfumo wa kuamini ushirikina katika uchimbaji,
“Nilienda kwenye ziara mkoa mmoja wapo hapa Tanzania sitaki kutaja nikaja kupata mgogoro,wanakitu kinachoitwa kusafisha duara,wanatafuta mamammoja wanamlipa pesa anashuka kule kwenye duara akiwa utupu kwa imani kuwa akisha toka madini yataonekana,lazima tuwahamishe watanzania kwenye imani hiyo”Alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Profesa Justinian Ikingula, yeye amekiri kupoeka na kuahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Biteko kna kusema kuwa,wanatambua umuhimu wa rasilimali ya madini katika kukuza pato la Taifa na kuinua uchumi,
“Vilevile tunatambua nia na lengo la Serikali ya awamu ya tano inayoongoizwa na Mh.Ris Dk.John Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa sekta ya madini inaendelea kukua na kutoa mchango mkubwa zaidi katika pato la Taifa”Alisema
Aidha pia majukumu ya Bodi hiyo yameainishwa kuwa ni pamoja na kutathimini utendaji kazi wa GST,Kupitisha bajeti ya Taasisi hiyo,kusimamia utekelezaji wa majukumu ya GST na kuhakikisha kuwa inajengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Pia imeelezwa kuwa,Bodi ya GST itafanya kazi yake kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo mara baada ya ukomo huo mjumbe yeyote anaweza kuteuliwa tena kuendelea na nafasi yeke endapo Mh,Rais pamoja na Waziri wa Madini wataona inafaa kwa manufaa ya Taasisi na Taifa kwa ujumla .

No comments:
Post a Comment