We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, March 28, 2019

KISA MFANYABIASHARA KUTEKWA, WAKENYA WAZUIA MAGARI YA TANZANIA

WAKAZI wa mpaka wa Kenya na Tanzania wa Namanga upande wa Kenya wamezuia magari kutoka Tanzania kuingia nchini mwao, kwa madai ya kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu wa kubadili fedha za kigeni wa nchini mwao hapo juzi Jumanne, Machi 26 majira ya saa 3 usiku.

Mmoja wa wananchi waliokuwa katika eneo hilo, Odinga Nguduu amesema kuwa, majira ya saa tatu ilikuja gari yenye namba za Tanzania kwenye Ofisi ya mfanyabiashara huyo na aliondoka naye kuelekea Namanga upande wa Tanzania.
“Tangu achukuliwe jana usiku hajarudishwa na hadi sasa haonekani mtu wetu, wakimrejesha tutaacha vurugu na tutaruhusu magari haya ya abiria na mizigo kuingia Kenya” amesema.

Naye Simon Ledupa Mkazi wa Namanga ya Tanzania amesema kuwa Namanga ni mpaka mkubwa na kuna watu wengi kutoka mataifa mbali mbali wanapita hapa, mtu huyu wanayedai ametekwa na Watanzania si kweli yupo humo humo kwao.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list