Ujenzi wa uwanja wa Simba ulioko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam ulisimama kwa muda kutokana na nyasi bandia za uwanja huo kushikiliwa na TAKUKURU kwa ajili ya uchunguzi wa kesi iliyokuwa ikiendelea
Hata hivyo Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema tayari TAKUKURU imeziachia nyasi hizo hivyo wakati wowote ujenzi wa uwanja huo utaendelea
Awali uwanja huo ulitarajiwa kukamilika mwezi wa pili lakini sasa baada ya nyasi hizo kuachiwa, Magori amesema ujenzi utakamilika baada ya wiki mbili
Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' aliahidi kuukamilisha uwanja huo tayari kuanza kutumika kabla ya msimu huu kumalizika

No comments:
Post a Comment