Tetesi zilizopo katika usajili ni kuwa beki wa pembeni wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Gadiel Michael imedaiwa kuondoka nchini kuelekea nchini Afrika Kusini kwaajili ya majaribio.

Gadiel Michael ambaye anakipiga kwenye klabu ya mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga imedaiwa amekwenda kufanya majaribio kwenye klabu ya Bidvest West ya Afrika Kusini.
Nyota huyo wa Taifa Stars anatarajiwa kuwa huko kwa muda wa wiki mbili kabla ya kurejea nchini.
No comments:
Post a Comment