We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, March 27, 2019

Burundi imewaachilia huru wanafunzi watatu wa kike, ambao walikamatwa kwa kosa la kuichafua kwa kuichorachora picha ya rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza

Burundi imewaachilia huru wanafunzi watatu wa kike ambao walikamatwa wakishutumiwa kuichafua kwa kuichorachora picha ya rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kwenye vitabu vyao vya shule.Waziri wa sheria Aimée Laurentine Kanyana ameeleza.



Kushikiliwa kwa wasichana hao takribani majuma mawili yaliyopita kwa shutuma za kumtusi rais kulizusha kampeni mitandaoni za kutaka wasichana hao waachiliwe kampeni iliyokua na jina #FreeOurGirls, watu wakituma picha kwenye mitandao ya Twitter.
Kwa mujibu wa BBC. Waziri amesema wasichana hao wenye miaka 15,16 na 17 wameachiwa huru kwa muda. ”Tunawataka wazazi kuboreha elimu ya watoto wao .Tunawakubusha watoto kuwa wanapaswa kuheshimu mamlaka,na kuwa umri wa kuwajibishwa ni miaka 15
Walikamatwa walipokuwa katika shule ya ECOFO iliyopo katika mkoa wa kaskazini wa Burundi wa Kirundo tarehe 12 mwezi Machi ,2019
Awali walishitakiwa wakiwa wanafunzi saba, lakini wanne wakaachiliwa huru.


mchoro
Image captionMchoro unavyoonekana

Watatu hao walikua wanashikiliwa kwenye gereza la wanawake la mkoa wa Ngozi.
Mnamo mwaka 2016 shule mbali mbali mjini Bujumbura na mikoani watoto kadhaa walitiwa mbaroni wakihusishwa na matukio ya aina hiyo.
Shirika la kutetea watoto FENADEB lilikua msitari wa mbele kuwatetea watoto hao.
Mashirika ya kutetea haki za watoto nchini Burundi yameshauri uchunguzi wa kina ufanyikekabla ya kuwatia watoto hao hatiani ili kubaini ni kwa nini matukio kama hayo yanajitokeza.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list