Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa aliikatia tamaa Timu ya Tanzania na kuhisi kuwa itafungwa huku akisema aliona ni vyema aangalie mpira akiwa ndani kuliko kwenda kupata fedheha.
Rais Magufuli amesema kuwa alipanga asiite Timu yoyote Ikulu, na hakuwahi kumtafuta Waziri Mwakyembe tangu iliposhindwa kipindi cha nyuma.
"Lilipofungwa goli la kwanza nilijua tu bado tutafungwa, mpaka lilipofika goli la tatu nikasema hapa tunafunga nikageukia Lesotho, Mke wangu aliniambia kuwa Tanzania leo tunafunga nikamwambia wewe unajua nini?, amesema Rais Magufuli.
Aidha amesema kuwa "Watanzania tunaweza ila tatizo ni moja,inawezekana baada ya kushinda jana viburi vimewajaa, najua mnapenda kupongezwa ngoja mimi niwatandike hapa hapa."
Rais Magufuli ameiita timu hiyo Ikulu, kufuatia jana kuifunga timu ya Uganda 3 bila na kufuzu AFCON 2019.

No comments:
Post a Comment