Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif ameeleza tofauti anayoiona yeye kati ya Zitto na viongozi wengine wa upinzani, amesema wote ni wazuri, ingawa Zitto na chama chake pamoja na uchanga wao wanajua kujenga hoja.
“Naona wote ni wazuri, pamoja na udogo wao na uchanga wao wewe mwenyewe ni shahidi jinsi wanavyoibua mambo mazito kwenye nchi hii, Zitto si mropokaji, anafanya kwanza utafiti akipata uhakika anasema, hata kama anajua wenye nguvu na mamlaka hawapendi na hiyo kaambukiza wengine wanaomfuata,” amesema Maalim Seif.
Aidha, anasema anaamini ACT-Wazalendo hakutakuwa na majungu wala makundi kama alikotoka na kwamba wao wanawaheshimu hata walioshiriki kuanzisha chama hicho na baadaye kuamua kujiunga na CCM.
“Kabla ya kwenda sisi kuna watu walikuwa waanzilishi, wakaamua kuacha jahazi na kwenda chama kinachotawala, jambo ambalo ni zuri, kwasababu ukiona hapa kuna sehemu nyingine nzuri ni jambo zuri sana.”

No comments:
Post a Comment