Simba imepania kwelikweli kuboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao! Hilo limedhihirika kutokana na michakato ya usajili kuanza mapema
Juzi Jacques Tuyisenge alikuwa nchini kumalizana na mabingwa hao wa Tanzania Bara akitarajiwa kujiunga nao mwishoni mwa msimu wakati huo huo nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib nae akiwa njiani kurejea nyumbani
Anayefuatia ni beki kisiki wa Azam Fc Yakubu Mohammed. Inaelezwa Yakubu tayari amefikia makubaliano ya awali na uongozi wa Simba na atamwaga wino mwishoni mwa msimu
Kakolanya nae safi
Mlinda lango wa Yanga Beno Kakolanya aliyegoma kuitumikia timu hiyo kutokana na 'ukata', nae anasubiri kumalizwa kwa mgogoro baina yake na uongozi wa timu hiyo
Kakolanya ameitaka Yanga ivunje mkataba wake na tayari ameliwasilisha suala hilo kwa TFF
Kakolanya anatarajiwa kujiunga na Simba akiwa mchezaji huru
Wakati huo huo Simba inaendelea kumjaribu kiungo mkabaji Jean Vital Ourega aliyetokea nchini Ivory Coast

No comments:
Post a Comment