Juhudi za kukuza soka barani Afrika zinaendela baada ya CAF kuzindua mafunzo ya matumizi ya usaidizi wa maamuzi kupitia video (VAR) jijini Johannesburg, Afrika kusini jumanne machi 26.
Mafunzo hayo ya siku tano yamepangwa kumalizika Machi 30 na kushirikisha waamuzi 21 na waamuzi wasaidizi 23 kutoka mataifa 32 mwanachama wa shirikisho la soka la Afrika CAF, ambapo wanajifunza kiundani namna ya kutumia teknolojia hiyo mpya kwenye kufanya maamuzi uwanjani.
Mkurugenzi wa bodi ya kimataifa ya sheria za mchezo (IFAB) David Elleray ambaye anaongoza mafunzo hayo, amesema waamuzi hao wamevutiwa na teknolojia hiyo na wanatizama mbele kuanza kuitumia kwenye ligi wanazochezesha hapa barani Afrika.

No comments:
Post a Comment