Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema Serikali itawafutia leseni waagizaji wakubwa wa pembejeo za kilimo watakaobainika kuingiza pembejeo na viuatilifu bandia kutoka nje bila kujali athari inazolisababishia taifa kwenye ukuzaji wa sekta ya kilimo.
Hasunga ametoa angalizo hilo jijini arusha kwenye kongamano linalowakutanisha maafisa ugani, watafiti na waagizaji wa pembejeo kujadili namna ya kuwasaidia wakulima kuepukana na matumizi yasiyo sahihi ya pembejeo na visumbufu vya mimea na mazao.
Akizungumzia hatua zinazochukuliwa kudhibiti uingizwaji holela wa pembejeo na viuatilifu hivyo bandia kaimu mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa viuatilifu nchini tpri dakta Magreth Mollel anasema wanakusudia kuongeza vituo vya ukaguzi mipakani.
Baadhi ya wazalishaji na wasamabazaji wa pembejeo za kilimo Suleiman Ally aliyehudhuria kongamano hilo wanaema uingizwaji holela wa bidhaa bandia kutoka nje ya nchi kunawafanya kushindwa kufanya uzalishaji wa tija.

No comments:
Post a Comment