Inaelezwa dili la kiungo Shiza Kichuya kutua Pharco Fc inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Misri, limeiingizia Simba kiasi cha Mil 200 kutokana na mauzo ya mchezaji huyo
Kichuya alifuzu vipimo vya afya katika klabu hiyo juzi Jumatano na jana akasaini mkataba wa miaka miwili na kisha kutolewa kwa mkopo kwenda klabu ya ENPPI inayoshiriki ligi kuu nchini Misri
Kichuya tayari ameanza kujifua na klabu ya ENPPI ambayo inajiandaa kuikabili Al Ahly kwenye mchezo wa ligi kuu ya Misri Jumanne ijayo
Simba imeliondoa jina la Kichuya katika orodha ya wachezaji wake ambao wataivaa Al Ahly kesho katika mchezo wa ligi ya mabingwa
No comments:
Post a Comment