Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, January Makamba ametolea ufafanuzi juu ya ubaguzi wa ajira katika taasisi za muungano.
Makamba alikuwa anajibu swali la Mbunge wa Welezo, Saada Mkuya (CCM) ambaye alitaka kujua ni ajira ngapi zinapatikana kwa Wazanzibar kupitia makubaliano ya kutatua kero za Muungano.
Waziri Makamba amesema hakuna yeyote atakayapata kazi ya kukosa kutoka anatokea upande fulani wa Muuungano, na kazi zimekuwa zikitolewa kwa wote.
"Hakuna mtu yeyote, Mtanzania yeyote atakayepata kazi au kukosa kazi kwenye taasisi ya Muungano sababu anatoka upande mmoja au mwingine," amesema.
Ameendelea kwa kusema, 'Na nidhairi kwamba Wazanzibar wengi pia wanapata fursa katika taasisi ambazo hata sio za Muungano kwa sababu kwenye nafasi za ajira kwenye wizara na taaisisi zisizo za Muungano wana nafasi za kupata kazi hizo kwa sababu ni watanzania na wapo wanaofanya kazi hizo,'.
No comments:
Post a Comment