Msanii wa muziki na CEO wa Wasafi, Diamond Platinumz amesema tabia inayofanywa na baadhi ya wasanii ya kuhonga ili kazi zao ziweze kurushwa katika runinga yake hapendi na ametoa onyo endapo atakutana na msanii wa namna hiyo atamfunga kazi yake kuruka katika media yake ya Wasafi TV na Radio.
Hivyo amewataka wasanii kutumia Wasafi TV na Radio bure kurusha kazi zao kwani lengo kubwa la kuanzishwa kwa media hiyo ni kuhakikisha kazi za wasanii hapa nchini zinafika mbali.
Diamond Platinumz amezungumza hayo katika mkutano wa wasanii wa filamu na muziki ulioandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda jana.
Msikilize hapa chini, ambapo mbali na hayo pia ametoa ushauri kwa Mkuu wa Mkoa utaosaidia wasanii wenzake katika kufikisha kazi zao za sanaa mbali.
Tazama na sikiliza hapa.
No comments:
Post a Comment