Baada ya malamiko kuwa mengi kwa bodi ya Ligi kuhusiana na mpangilio wa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania bara kuwa inaziumiza baadhi ya timu ambazo zinalazimika kwenda na kurudi ndani ya mkoa mmoja mara mbili kwa kipindi kifupi kwa ajili ya kucheza na timu nyingine.
Mfano mashabiki wa Yanga na wadau wa soka walikosoa kitendo cha Yanga kwenda kucheza Tanga na Coastal Union halafu ilasafiri kwa basi hadi Singida kucheza na Singida United baada ya siku tatu ikalazimika kurudi tena Tanga kucheza dhidi ya JKT Tanzania ambao nao wanautumia uwanja huo kama uwanja wa nyumbani.
Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura ametolea ufafanuzi kuhusu upangaji wa ratiba ya Ligi hiyo na kujibu kuhusu tuhuma hizo na malalamiko “Ligi haiwezi kuchezwa upande mmoja sasa timu mmoja ikienda upande huo ikae wee sasa hiyo itakuwa sio Ligi sasa Ligi haiwezi kuwa kama Ligi ya Zanzibar yaani zinacheza Unguja halafu baadae zinaamia Pemba haziwezi kuwa katika mfumo huo”>>>Boniface Wambura
CHANZO: AZAM TV
No comments:
Post a Comment