Nahodha wa zamani wa club ya Chelsea John Terry ameamua kufunguaka na kueleza mtazamo wake kuhusiana na kitendo cha golikipa wa Chelsea Kepa Arrizabalag kumgomea Kocha Maurizio Sarri kumfanyia mabadiliko na kumuingiza Caballero katika mchezo wa fainali ya EFL Cup kati ya Chelsea dhidi ya Man City.
Kitendo hicho ambacho kilitokea dakika ya 119 dakika moja kabla ya mchezo wa fainali kumalizika na mikwaju ya penati kuchukua nafasi, Terry ambaye amewahi kuwa nahodha wa Chelsea kwa miaka kadhaa amekosoa kitendo cha Kepa na kusema kuwa hata kama alikuwa anajua kocha alitaka kumtoa kwa kudhani kaumia hakutakiwa kugoma ilipaswa kukubali kutoka ndio aeleze malalamiko yake.
“Kibao cha kufanya mabadiliko kinapooneshwa unapaswa kukubali kutoka uwanjani na kuonesha heshima kwa kocha, baada ya kutoka ndio ueleze malalamiko yako ambacho ndio kitu cha mwisho mchezaji anatakiwa kufanya”>>>John Terry
Hata hivyo Kepa alitoa kauli ya kujitetea kuwa aligoma kutoka kwa sababu alidhani kocha wake Maurizio Sarri alitaka kumtoa akiamini alikuwa na majeraha lakini yeye alikuwa anafanya vile ili kupoteza muda tu na kuufanya mchezo uende ukaamuliwe na mikwaju ya penati, hata hivyo changamoto ya mikwaju ya penati iliipa Man City Ubingwa wa penati 4-3.
No comments:
Post a Comment