Jana Yanga ililazimika kutokea nyuma mara mbili na kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Biashara United kwenye mchezo wa kombe la FA kabla ya kuibuka na ushindi kupitia changamoto ya mikwaju ya penati
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewasifu wachezaji wa timu yake kwa kupambana mpaka wakapata matokeo yaliyowapeleka raundi ya tano ya michuano hiyo
"Wachezaji nawapongeza kwani wamepambana. Mara zote walipofungwa hawakukata tamaa, walirudisha mabao na baadae kushinda kupitia mikwaju ya penati," amesema
"Biashara United ni timu nzuri, wanajilinda vizuri na wanapanga mashambulizi vizuri. Tulifahamu mchezo hautakuwa mwepesi kwani tayari tulishacheza nao kwenye ligi"
Yanga itachuana na Namungo Fc katika mchezo wa hatua ya 16 bora utakaopigwa mkoani Lindi, Wilaya ya Ruangwa
Mwezi Novemba 2018 Yanga ilicheza na Namungo Fc mchezo wa kirafiki katika dimba la Majaliwa na kulazimishwa sare ya bao 1-1
Kocha Zahera hakusafiri na Yanga kwenye mchezo huo kwa kuwa alikuwa na majukumu ya timu ya Taifa
No comments:
Post a Comment