KLABU ya Real Madrid bado haijakata tamaa katika mchakato wake wa kuwania kumsajili mshambuliaji Marcus Rashford ambapo ipo tayari kutoa pauni 100m (Sh bilioni 302) ili kumsajili.
Straika huyo bado yupo kwenye mazungumzo ya mkataba mpya klabuni kwake Manchester United ambapo amekuwa akionyesha kiwango kizuri katika michezo ya hivi karibuni.
Taarifa hizo zimekuja wakati ambapo staa mwingine wa timu hiyo, Anthony Martial akiwa amekubali kusaini mkataba mpya wa miaka mitano kuendelea kubaki United. Hatua hiyo imewafurahisha mabosi wa United ambao wanaamini huo unaweza kuwa ushawishi mzuri kwa Rashford naye kusaini mkataba mpya.
Rashford, 21, hakuwa na furaha chini ya kocha aliyefukuzwa Jose Mourinho lakini kwa sasa anaonyesha kuwa na makali na ni mchezaji anayejiamini zaidi chini ya kocha Ole Solskjaer.
Mkataba wake wa sasa analipwa pauni 60,000 (Sh milioni 181) kwa wiki lakini taarifa zinaeleza kuwa kwa kuwa Madrid wameonyesha nia ya kutaka kumsajili, basi kuna uwezekano wa kuongezewa mshahara wake na kuwa pauni 200,000 (Sh milioni 604) kwa wiki.
Chini ya Solskjaer, Rashford amefu-nga mabao ma-tano katika mich-ezo saba aliyoa-nza.
No comments:
Post a Comment