Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini hawezi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kufafanua kauli yake au kutaja sababu hasa itakayopelekea kiongozi huyo na chama chake kushindwa kushika dola.
Kauli hiyo ya Spika ameitoa Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kujadili muswada wa vyama vya siasa nchini ambapo aliingilia kati uchangiaji Waziri wa zamani wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene ambaye alikua akichangia.
Katika mchango wake Simbachawene alitolea mfano kiongozi huyo wa ACT - wazalendo kuwa Rais wa nchi lakini akihoji itakuaje kama akishuhudia wapinzani wake wakiendesha shughuli za maandamano.
Wakati Simbachawene akizungumza ghafla Spika wa Bunge Job Ndugai aliingilia kati na kusema, "mheshimiwa Simbachawene bahati nzuri Zitto hawezi kuwa Rais wa nchi haiwezekani."
Kupitia ukurasa wake wa Twitter kujibu kauli hiyo Zitto ameandika, "namuomba sana Mungu ampe uhai Job Ndugai na pia anipe uhai na kama kuna kheri ndani yake anipe nafasi ya kusaidiana na wenzangu kuongoza nchi yetu, hakuna ajuaye ya kesho isipokuwa Mungu tu".
No comments:
Post a Comment