Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa rufaa ya kupinga dhamana iliyokatwa na upande wa mashtaka dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko itaanza kusikilizwa Februari 18, 2019 katika Mahakama ya Rufaa.
Hayo yameelezwa leo Alhamisi na wakili wa Serikali, Wankyo Simon mbele ya hakimu mfawidhi, Kelvin Mhina wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Wankyo amedai kuwa kesi lilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba wanasubiri uamuzi wa mahakama ya rufaa.
Amedai kuwa rufaa hiyo ya kupinga dhamana iliyokatwa na upande wa mashtaka itaanza kusikilizwa Februari 18, 2019.
Hakimu Mhina baada ya kusikiliza hoja za pande zote , ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 14, 2019 itakapotajwa.
Mbowe na Matiko ambaye pia ni mhazini wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) wanaendelea kusota rumande kutokana na kufutiwa dhamana.
Leo kwa mara ya kwanza tangu Mbowe na wenzake wafikishwe mahakama ya Kisutu, aliyekuwa waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu alikuwepo mahakamani hapo na kushuhudia Freeman Mbowe Akirudishwa Gerezani
No comments:
Post a Comment