Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda ameagiza vyombo vya usalama kumchunguza msanii Harmonize kama anatumia bangi au lahh! ili achukuliwe hatua za za kisheria.
Makonda ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 31,2019 wakati akizungumza na wasanii katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Amesema katika mtandao wa Instagram ameona picha ikimuonyesha Harmonize anayetamba na wimbo Paranawe akivuta kitu hicho hivyo ameomba ichunguzwe kama ni bangi au lah.
“Nimemuagiza Gavana wa huko achunguze ile ni bangi au nini na ikigundulika ni bangi atakapotua tu hapa ni pingu na kupelekwa lock up, Vizuri namlea mwenyewe na mtoto anapokosea lazima umshikishe adabu bila kujali unampendaje,” amesema Makonda.

No comments:
Post a Comment