Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Kaimu Mwenyekiti wake Samuel Lukumay umesema tayari ulimshamlipa stahiki zake mlinda lango Beno Kakolanya hivyo mchezaji huyo haidai Yanga kwa sasa
Aidha Lukumay amekiri Yanga kupokea barua ya Mwanasheria wa Kakolanya akiomba kuvunja mkataba wa mteja wake na amesema uongozi wa Yanga utakaa kulijadili ombi hilo
Lukumay amesema Kakolanya ni mchezaji halali wa Yanga kwa kuwa bado ana mkataba wa miaka miwili hivyo kama anataka kuvunja mkataba wake inafaa akafuata taratibu za kisheria
Aidha kuhusu hatma yake ya kurejea Yanga, Lukumay amesema mlinda lango huyo alipaswa kuwasili na uongozi wa Yanga na kocha Mwinyi Zahera ili kupata ufumbuzi wa sintofahamu iliyojitokeza lakini hakufanya hivyo
Kakolanya hataki kurudi Yanga
Kwa wale wanaomlaumu kocha Mwinyi Zahera kumuengua Beno, kwa kauli hii ya Lukumay nadhani watakuwa wamepata picha juu ya nini kinaendelea
Inaonekana uongozi wa Yanga ulikuwa tayari kumsamehe Beno ili aendelee na majukumu yake lakini yaonekana mgomo wake ni wa kutaka kuondoka Yanga
Kwani licha ya kuwa amelipwa stahiki zake, bado ameshikilia msimamo wa kutaka kuvunja mkataba wake
No comments:
Post a Comment