Msaniii wa Bongo Fleva, Barnaba amesema ni kweli msanii wa filamu Bongo, aliponunua albamu yake ya Gold kwa US Dollar 3,000.
Muimbaji huyo ameeleza hayo kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM ambapo ameeleza kuwa fedha hizo alikuja kupatiwa kwa hawamu mbili.
"Asubuhi alituita ofisini kwake, nikiwa na boss wangu alitulipa Dola 2000, na baadae wakati tunafanya video ya Washa aliongezea ile Dola 1,000 iliyobakia kama mchango wake kwenye video, hivyo amehusika pia kwenye video," ameeleza Barnaba.
Utakumbuka 31 August 2018 katika uzinduzi wa albamu ya Barnaba 'Gold', msanii wa Filamu Bongo, Jackiline Wolper alinunua nakala moja ya albamu ya hiyo kwa US Dollar 3,000 sawa na Tsh. 6,860,536 (Mil 6).
"Siku hizi nimekuwa Bosslady, sio Wolper tena, hivyo Albamu ya Barnaba nitanunua kwa Dola 3,000," alisema Wolper.
No comments:
Post a Comment