Uongozi wa klabu ya Yanga umewashukia wanaopotosha na kuripoti taarifa za uongo kuhusu klabu hiyo zenye lengo la kuvuruga utulivu uliopo
Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Yanga Siza Lyimo amesema baadhi ya magazeti hasa la Tanzanite limekuwa likiandika habari za uongo kuhusu klabu ya Yanga
Amesema gazeti hilo limekuwa na mfululizo kuandika habari ambazo hata chanzo chake hakifahamiki.
Amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo waendelee kuwaamini viongozi wao
"Tunaandamwa na wimbi la watu wasioitakia mema klabu ya Yanga. TunawatakaWanachama na mashabiki wenye mapenzi mema na klabu yao wawaamini viongozi wao"
Aidha Siza amesema wapo watu wamekuwa wakimtumia meseji za vitisho na kumtukana kocha Mwinyi Zahera.
"Tunalaani wote wale wanaotumia mitandao vibaya kwa kuwatukana viongozi wa Yanga na Mwalimu Zahera.
'Tunalaani wote wanaomtumia Mwalimu meseji za matusi na vitisho na tunawataka waache mara moja kwa sababu wao sio zaidi ya Mwalimu"
No comments:
Post a Comment