Mbunge wa Chemba Juma Nkamia, ameeleza katika jimbo lake wananchi wa wanakabiliwa na balaa la njaa, kufuatia baadhi ya Maafisa wa Serikali kuwataka kutupa vyakula, ambavyo vilidaiwa kuwa na ugonjwa wa Sumu Kuvu.
Mbunge Nkamia ametoa kauli hiyo wakati uzinduzi wa mpango wa Kilimo cha Matunda na Mbogamboga mkoani Dodoma, ambapo kiongozi huyo alibainisha kuwa tangu Serikali iwatake wananchi hao, watekeleze agizo hilo halijafanya jitihada zozote za kuwasaidia.
Nkamia amesema kuwa "Serikali ilikuja kuwaambia wananchi wamwage vyakula, watu walimwaga mahindi na magunia mengi ila leo wanalia njaa, na imetuachia mimi na Mbunge mwenzangu wa Kondoa, siyo jambo jema."
Mbunge Juma Nkamia alishawahi kupendekeza Bungeni kuongezwa kwa muda kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, kwa kile alichokidai kuepuka gharama za uchaguzi.
No comments:
Post a Comment