Usiku wa October 1 2019 ulikuwa ni usiku wa muendelezo wa game za hatua ya makundi ya michuano ya UEFA Champions League, usiku huo zilichezwa game nane za makundi lakini game iliyokuwa gumzo mtandaoni ni game ya Tottenham Hotspurs dhidi ya FC Bayern Munich ya Ujerumani, game hii imechezwa London katika uwanja wa Tottenham Hotspurs.
Wakati game hii inaanza haikuwa inawekewa uzito sana kutokana na timu zinazocheza sio kubwa sana na hazina mashabiki sana kwa ukanda wa Afrika Mashariki, baada ya kuanza kuchezwa na Tottenham Hotspurs kuruhusu goli nyingi ndipo gumzo likaibuka na watu kuanza kuifuatilia ili kujua makamu Bingwa wa UEFA Champions League msimu uliopita kwa maana mshindi wa pili kapatwa na nini.
Magoli ya Joshua Kimmich dakika ya 15, Robert Lewandowski aliyefunga mawili dakika ya 45 na 87 pamoja na Serge Gnabry aliyefunga hart-trick dakika ya 53, 55, 83 na 88 na kuufanya mchezo umalizike kwa magoli 7-2, huku Spurs wakifunga mawili kupitia kwa Son Heung-Min dakika ya 12 na Harry Kane kwa mkwaju wa penati dakika ya 61 kunaifanya Tottenham Hospurs kuingia katika rekodi mbaya ya kuwa hiko ndio kipigo chao kikubwa cha kwanza katika historia yao kufungwa katika game yao ya nyumbani.
No comments:
Post a Comment