We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, October 2, 2019

Samatta kuipa ushindi wa kwanza UEFA klabu yake ya Genk leo mbele ya Napoli ?

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta usiku wa leo akiwa na klabu yake ya KRC Genk anatarajiwa kushuka dimbani kwa mchezo wake wa pili wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya (Champions League) dhidi ya Napoli.
Genk, itakuwa nyumbani Ubelgiji katika dimba la Luminus Arena ikiwakaribisha miamba kutoka Italia klabu ya Napoli.
Katika mchezo wake wa kwanza Genk iliangushiwa kichapo kizito cha goli 6-2 ugenini dhidi ya RB Salzburg, huku Samatta akifunga goli moja la kufutia machozi.
Katika mchezo huo, Samatta aliweka rekodi binafsi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Champions League na kufunga goli. Napoli wao walianza kwa kuwafunga mabingwa watetezi Liverpool goli 2-0.
Hivyo, Genk hii leo watakuwa tena na kibarua kizito cha kuwazuia Napoli.

 

Hata hivyo, japo Genk haijawahi kupata ushindi hata mechi moja ya Champions League katika mara zote tatu walizoshiri michuano hiyo, wamefungwa mechi moja tu nyumbani kati ya sita walizocheza na kutoka sare tano.
Napoli pia hawajapata ushindi wakiwa ugenini kwenye hatua ya makundi ya Champions League katika mechi sita zilizopita. Hivyo, japo si ya kutumainia, historia inaweza kuwabeba Genk na kupata walau sare.

Kalidou Koulibaly
Image captionKalidou Koulibaly alimkaba Samatta vilivyo Senegal ilipoifunga Tanzania 2-0 kwenye micuano ya Afcon.

Mechi ya leo pia itawakutanisha tena Samatta na beki kisiki Kalidou Koulibaly raia wa Senegal.
Wawili hao waliminyana kwenye michuano ya Afcon Juni 23mwaka huu ambapo Senegal ilipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Tanzania.
Je, Samatta ataweza kumpita Koulibally leo na kufunga goli baada ya kushindwa kufurukuta mbele yake Afcon?
Mechi hiyo itapigwa kuanzia saa mbili kasoro dakika tano za usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list