Mshambuliaji wa Manchester United na Chile Alexis Sanchez, 30, amesema "ameyapata tena mapenzi yake ya kucheza mpira" baada ya kujiunga kwa mkopo na Inter Milan. (Eurosport)
Manchester United wanataka kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Lyon Moussa Dembele, 23, na kiungo wa Newcastle Sean Longstaff, 21, mwezi January. (Star)
Barcelona wanajipanga kutuma tena ofa ya usajili kwa kiungo wa Chelsea na Brazil Willian, 31, ambaye bado hajasaini mkataba mpya na Chelsea, na alionao unaisha mwishoni mwa msimu. (Mundo Deportivo via Express)
Mshambuliaji wa Burnley Jay Rodriguez, 30, anahusishwa na tetesi za kushtukiza za uhamisho kuelekea klabu ya Inter Milan mwezi Januari. (Calcio Mercato via Sport Witness)
Kocha wa zamani wa Juventus Mtaliano Massimiliano Allegri, 52, anajifunza Kingereza akilenga kuhamia katika Ligi ya Primia, husussan klabu ya the Manchester United. (Guardian)
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp atasikitishwa sana iwapo watalazimishwa kucheza mchezo wa marudiano wa Kombe la Corabao dhidi ya MK Dons kama adhabu ya kumchezesha mchezaji asiyestahili. (Times)
Mshambuliaji wa Tottenham na Korea Kusini Son Heung-min, 27, amesema kuwa alitaka kuihama klabu hiyo mwaka 2016 lakini akashawishiwa kubaki na kocha Mauricio Pochettino. (Goal)
Kocha wa Newcastle United Steve Bruce amewauliza kwa hasira wachezaji wake iwapo wanataka kuendelea kuichezea klabu hiyo kwa moyo mmoja baada ya kupokea kichapo cha goli 5-0 dhidi ya Leicester. (Telegraph)
Mlinzi wa zamani wa Man United na timu ya taifa ya England Rio Ferdinand amependekeza kuwa mshambuliaji wa klabu ya Tottenham na timu ya taifa ya England Harry Kane, 26, ahame klabu yake iwapo anataka kushinda mataji makubwa. (Mail)
Beki wa England England Kieran Trippier, 29, amesema "sikujiuliza mara mbili" juu ya kuihama Tottenham yenye maskani yake Kaskazini mwa London na kujiunga na klabu ya Atletico Madrid ya Uhispania. (Football.London)
Atletico Madrid wamefanya mazungumzo na klabu ya Al Rayyan ya Qatar juu ya usajili wa mshambuliaji Diego Costa. (AS Diario via Mail)
Everton wameshindwa kumsajili mshambuliaji kinda wa Ureno Rafael Leao licha ya kutoa kitita cha euro milioni 30. Klabu ya Lille ilimuuza mshambuliaji huyo AC Milan. (Tuttosport via Liverpool Echo)
No comments:
Post a Comment