Kiungo Mapinduzi Balama amejumuishwa kwenye kikosi cha Yanga kilichoingia kambini kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania
Mchezo huo utapigwa kesho Alhamisi kwenye uwanja wa Uhuru
Balama amekuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili akiuguza majeraha ya nyama za paja aliyopata kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United
Kurejea kwa kiraka huyo ni habari njema kwa kocha Mwinyi Zahera ambaye kesho kikosi chake kitashuka dimbani kusaka ushindi wa kwanza ligi kuu ya Vodacom msimu huu
No comments:
Post a Comment