Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, ambaye yuko chini ya lebo kubwa ya muziki hapa Tanzania ya WCB ambayo inasimamiwa na Diamond Platnumz Rayvanny, ameitumia siku ya leo ikiwa ni birthday ya Boss wake Diamond kumuandikia ujumbe mzito ambao umeambatana na maneno ya kumtia moyo.
Rayvanny ameandika hivi: “MUNGU ALIKUCHAGUA UKAWE KIONGOZI , KIONGOZI HANA TOFAUTI NA DEREVA WA GARI . YANI ABIRIA MNAWEZA KULALA USIKU KUCHA, YEYE HALALI KUHAKIKISHA MNAFIKA SALAMA MNAPOENDA. UMEASAIDIA WENGI SAAAANA NA BADO UNAWASAIDIA WENGI SANA LAKINI PIA WAPO WANAOTAMANI MSAADA WAKO PIA. WEWE NI KIONGOZI , KUTUKANWA, KIDHALILISHWA, KUSIMANGWA , KUONEKANA UNA MATATIZO NISEHEMU YAKO YA KAZI MAANA LAWAMA SIKUZOTE NI ZA KIONGOZI ,YANI YULE ANAE KAA MBELE SIKU ZOTE NI WAKULAUMIWA TU. NAOMBA MTANGULIZE MUNGU KATIKA MAWAZO NA KILA ULIFANYALO MAANA BINADAMU SIO WOTE WANAOPENDA MAFANIKIO YAKO……… NAAMINI WENGI WANAKUPENDA HATA WANAOKUTUKANA WANAKUPENDA , HATA AMBAO WATU WANAHISI NI MAADUI ZAKO BADO WANAKUPENDA SANA . MATATIZO UNAYOKUTANA NAYO NAOMBA YASI KUKATISHE TAMAA NA KUKUVUNJA MOYO WA KUSAIDIA WENGINE…….. HAPPY BIRTHDAY BIG @Diamondplatnumz”
No comments:
Post a Comment